Wamola: “Asilimia 75 ya waafrika bado wanahitaji simu za mkononi”
Viongozi mbali mbali wa mashirika ya mawasiliano ya simu za mkononi (Mobile World Congress) barani Afrika, walikutana mjini Kigali kuanzia tarehe 17 hadi 19 Octoba 2023.
Viongozi wanasema kuwa Bara la Afrika lina changamoto kubwa kuhusu utumiaji wa teknolojia ya mawasiliano.
Angela Wamola ni Mkurugenzi wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ( GSMA), akiongea na brightafrica.rw amesema kwamba mkutano huo ulikuwa unalenga maendeleo kwa Bara la Afrika, kujadiliana miaka 10 iliyopita kulingna na Umoja wa Afrika, Agenda 2023.

Bi Wamola amesema kwamba kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita idadi ya wananchi wanaotumia simu za mkononi imeongezeka hususan kwa kutumia Mobile money, ambayo imewasaidia barani Afrika,
Amesema “ Tunaweza kusema kwamba Mobile money imeweza kusaidia watu kufungua akaunti hususan wale ambao hawakuwa na uwezo wa kufungua akaunti kwenye simu zao. Hiyo akaunti ni sambamba na kufungua akaunti kwenye benki’’.
Amebaini kwamba watu wanaweza kupata pia mikopo na kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Aidha, Wamola amesema kwamba katika mkutano wa Kigali, walijadiliana kwa pamoja uwezekano wa kutumia teknolojia ya sekta ya elimu, kilimo, afya pamoja na biashara barani Afrika kwa ujumla, isiwe katika ukanda wa Afrika ya mashariki peke yake.
Ameongeza kuwa watashirikiana na kuwa na sauti moja kuhusu sekta ya mawasiliano. Hata hivyo idadi ya watu wanaotumia simu za mkononi, pamoja na kwamba imeongezeka,lakini bado kuna changamoto.
Wamola amesema “ Kile ambacho wananchi wanasema, wangependa tuwasaidia wapate simu za mkononi. Tukiangalia asilimia 25 wamepaa hizi simu ambao zina uwezo wa kupta mawasiliano ya na mtandao (Internet). Kuna Asilimia 75 ya watu wetu ambao hawajapata uwezo wa kupata simu za mkononi ili wanufaike kwa mawasiliano ya mtandao’’,

Viongozi mbali mbali walishiriki vikao vya mawasiliano jijini Kigali.
Kuhusu utumiaji wa mawasiliano ya simu nchini Rwanda, mpaka sasa kuna asilimia 82 ya wafanyakazi wanaotumia simu za mkononi, asilimia 20 wana smart phone, wenye ujuzi katika utumiaji wa teknojia ni asilimia 35,1 wakati Malengo ni kufikia asilimia 60 mwakani 2024. Hata hivyo safari bado ni ndefu katika bara la Afrika kwa watu wanohitaji mawasiliano ya simu za mkononi.

GSM ni shirika ambalo linawakilisha maslahi ya waendeshaji wa mtandao wa simu duniani kote. Zaidi ya waendeshaji 750 wa simu ni wanachama kamili wa GSMA na makampuni zaidi 400 katika mfumo mpana wa ikolojia ya simu.
Christopher Karenzi
