Mashindano ya mpira wa wavu (volleyball): Police, APR, REG na Kepler zapata ushindi katika Mashindano ya Afrika 2026

Share Now

Na Christopher Karenzi

Timu nne zinazoiwakilisha Rwanda katika Mashindano ya Afrika ya Klabu Bingwa za Volleyball—APR VC, Kepler VC, Police VC na REG VC, zimefanya vizuri katika michezo ya siku ya tatu ya mashindano haya yanayoendelea jijini Kigali.

Michezo hiyo inayofanyika katika ukumbi wa BK Arena na Petit Stade, iliendelea Ijumaa tarehe 24 Mei 2026, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Michezo, Nelly Mukazayire, na Waziri wa Afya, Dkt. Sabin Nsanzimana, pamoja na Rais wa CAVB Bi Bouchra Hajij  na wengine wengi.

APR VC ilishinda Litto Team ya Cameroon kwa seti 3-0 (17-25, 18-25, 22-25), huku Kepler VC nayo ikiibuka na ushindi dhidi ya Sports-S ya Uganda kwa seti 3-0 (25-22, 25-17, 25-20). Timu hizi mbili zilipata ushindi wao wa pili mfululizo katika mashindano haya.

Mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu uliwakutanisha Police VC na FUS Rabat kutoka Morocco, ambayo inashiriki mashindano haya kwa mara ya tatu. FUS Rabat ilianza vizuri kwa kushinda seti ya kwanza kwa alama 25-19 dhidi ya Police VC.

Katika seti ya pili, Police VC ilirejea kwa nguvu na kushinda kwa alama 28-26. Iliendelea kucheza vizuri katika seti ya tatu, ambapo wachezaji kama Matheus Bettim na Makuto Elphas walifanya vizuri katika kufunga pointi. Police VC ilishinda seti hiyo kwa alama 25-20.

Aidha, Police VC ilichukua pia seti ya nne kwa alama 25-21, hivyo kupata ushindi wake wa pili katika mashindano haya.

Katika mchezo uliotangulia, REG VC ilipata ushindi wake wa kwanza baada ya kuifunga Rukinzo VC ya Burundi kwa seti 3-0 (25-22, 25-15 na 25-22).

APR VC ilishinda Litto Team ya Cameroon kwa seti 3-0 (17-25, 18-25, 22-25), huku Kepler VC nayo ikiibuka na ushindi dhidi ya Sports-S ya Uganda kwa seti 3-0 (25-22, 25-17, 25-20). Timu hizi mbili zilipata ushindi wao wa pili mfululizo katika mashindano haya.

Mashindano yameeendelea Jumamosi, ambapo saa mbili asubuhi Police VC imecheza na Wolaita ya Ethiopia, wakati REG VC itacheza na General S ya Kenya. Kuanzia saa sita mchana, Cameroun S itacheza na Kepler VC, na saa nane mchana APR VC itakutana na Nemo Stars ya Uganda.

Bi Bouchra Hajij, Rais wa CAVB katikati

Waziri was michezo Nelly Mukazayire Katika katikati , Waziri wa Afya, Dkt. Sabin Nsanzimana Kushoto


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *