Ntore na Mpoyo waitwa kambini katika timu ya Taifa ya Rwanda

Share Now

Timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya Rwanda wanaume  yaitwa kambini kujiandaa safari kuelekea Morocco kusaka tikiti ya kombe la AfroBasket 2025.

Ntore na Mpoyo ni miongoni mwa wachezaji wa club ya jeshi la taifa APR BBC walioitwa kambini kujiunga na Timu ya taifa ya mpira wa kikapu kuelekea Morocco kusaka tikiti ya  fainali za FIBA AfroBasket zitakazofanyika tarehe 12 hadi 24 Juni 2025 nchini Angola.

Mechi za kundi lao zimepangwa kuanzia  tarehe  21 hadi 23 Februari 2025 nchini Morocco.

Rwanda ipo kwenye nafasi ya tatu katika kundi C na  alama 4 ikiwa nyuma ya Senegal na Cameroun,  Gabon ikiwa ya mwisho katika kundi hili.

Timu ya Rwanda itaondoka Kigali tarehe ijumaa tarehe 14 mwezi huu wa februari 2025 kuelekea Morocco.

Mpoyo akiwaponyoka wachezaji wawili

Kuhusu wachezaji hawa 2 ambao hawakucheza mechi iliyopita,  Kocha msaidizi wa APR BBC Aimé Nkusi Karim amesema  mchezaji Axel Mpoyo alikuwa amepata majeraha.  Ni jambo la kufurahisha kuwa ameitwa kujiunga tena kwenye timu ya taifa ya Rwanda pamoja na mwenzake Ntore.

Karim amesema ‘’Tuna timu ya taifa ni  nzuri  wachezaji maarufu  aina Mpoyo, Ntore na wengine hawakushiriki mechi iliyopita,  lakini leo wamerejea naamini kikosi ni kizuri wana Kocha imara Sir nafirkiri watapata ushindi huko Morocco’’.

Kocha  Aimé Nkusi Karim

 Aidha Kocha  Aimé Nkusi Karim amebaini kuwa kuhusu mchezaji machachari Mpoyo, alikuwa na jeraha takriban miezi 12 hachezi lakini wakati huu baada ya kutibiwa na kupona kiwango chake kinaridhisha.

Kwenye mechi ya APR BBC dhidi ya UGB  iliyopigwa kwenye uwanja wa mahoro maarufu Petit Stade,  Mpoyo aliongoza kwa ufungaji akiwa na alama 27. APR BBC  isiku hiyo jumapili tarehe 09.02.2024 iliifunga UGB kwa vikapu  86-61.

 Mbali na Ntore Habimana na Axel Mpoyo wa APR BBC, wengine waliotwa kwenye timu ya taifa ni pamoja na Nahodha Ndizeye Dieudonné wa MAS Basketball akiwa nchini Moroc, Hagumintwari Steven na Furaha Cadeaux de Dieu kutoka club ya Patriots, Muhizi Prince wa timu ya Nishati REG BBC na Bigirumwami Noah.

Kadhalika wameitwa William Robynes, Nshobozwabyosenumukiza Jean Jacques Wilson na Shema Osborn wa APR BBC.

Mpoyo Axel kushoto akimudhibiti vizuri mchezaji machachari wa Tigers

Hayo yakiarifiwa  wachezaji Antino Jackson wa APR BBC na Shema Bruno wa Tigers BBC wameitwa kambini kwa mara ya pili kwenye timu ya taifa ya mpira wa kikapu. Mashindano haya yanafanyika kwenye makundi 4. Kila timu itakutana na mwenzake halafu  timu tatu za kwanza zitapata tikiti ya kusonga  kwenye hatua ya fainali za FIBA AfroBasket, ambapo zimepangwa kufanyika tarehe 12 hadi 24 Juni  2025.

  Timu ya taifa ya Rwanda

Christopher Karenzi


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *