Mwingereza Joseph Blackmore kutoka Club ya Israel Premier Tech  atawazwa bingwa wa Tour du Rwanda 2024

Share Now

Shindano la kimataifa la Tour du Rwanda 2024 lililoanza  tarehe 18.02.204 limefikia kilele chake trehe 25 Februari 2024.

Nchi 19 kutoka mataifa mbali mbali duniani zilishiriki. Mwingereza Joseph Blackmore kutoka Club ya Israel Premier Tech  ametawazwa bingwa wa mbio za baiskeli Tour du Rwanda mwaka 2024.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 ametawala hatua ya 8 na ya mwisho umbali wa kilomita  73.3  katika  baadhi ya mitaa ya jiji la Kigali. Blackmore   ametumia  muda wa  saa 1 dakika 37 na sekunde 30 akifuatwa na mfaransa  Pierre Latour  wa TotalEnergies.

Mnyarwanda aliyekuja karibu  ni Moise Mugisha  wa timu ya Java-InovoTec  alimaliza  kwenye nafasi ya 12. Alikuwa nyuma kwa sekunde 46.

Kwa jumla mwingereza huyo ametawala mbio hizo umbali  wa kilomita 740 nchini Rwanda  baada ya kutumia muda wa  saa 17 dakika 18 na sekunde 46.

Walioshiriki shindano hili walikuwa zaidi ya 90 lakini waliofaulu kumaliza kinyang’ayro hicho walikuwa 63.

Blackmore amevikwa jezi ya manjano na Waziri wa michezo  Bi Aurore Mimosa Munyangaju.  Baada ya ushindi huo wa kwanza alikuwa na haya ya kusema ‘Kupanda milima imekuwa changamoto wapinzani wamekuwa wakali wakati nimefika sehemu ya kushuka na eneo tambarare nimewachosha, nimejaribu  kudhibiti muda wangu vizuri. Kwa mashindano yajayo  haa  tunakwenda kwenye maandalizi  tutaona cha kufanya’’ .

Mshindi wa awamu ya 16   Blackmore akishirikiana na bingwa mara nne  wa Tour  de France Christopher Froome  pamoja na wenzake  wa timu ya Club ya Israel (Israel Premier Tech) wameonyesha kiwango cha juu katika shindano hili.

Mnyarwanda aliyekuja karibu  ni Eric Manizabayo amekuja kwenye nafasi ya 15 akiwa nyuma kwa  dakika 5 na sekunde 13.

Mukasa Nelson ni Kocha wa kuongeza  nguvu za misuri katika timu ya May Stars ya  hapa nchini Rwanda, amesema kwamba timu yake bado ni changa katika mashindano kama haya ya Tour du Rwanda. Ina wachezaji mchanganyiko wakiwemo wanyarwanda na baadhi ya wachezaji wa kigeni.

Amebaini kuwa  wamejifunza mengi kutoka  kwa waendeshabaiskeli waliobobebea katika mshindano haya.

Kocha wa kuongeza nguvu za misuli katika timu ya May Stars Nelson Mukasa

Mukasa amesema: ‘’Tiimu zetu zinatakiwa kufanya michuano mingi ya ndani na ya kimataifa ili mwaka ujao timu za Rwanda ziwe kwenye kiwango kinachoridhisha’’

Mu eritria Dawit Yemane anayekipiga katika club ya Bike Aid ya Ujerumani ametawazwa kuwa mwendeshabaiskeli bora barani Afrika. Alikuwa na haya kusema. Amesema ‘’ Eh  kuna tufauti ya mashindano, mwaka jana lilikuwa gumu na mwaka huu limekuwa  gumu zaidi hususan wakati wa mbio za kufika kwenye mstali  (sprint) Kwa upande wangi mambo hayakuwa mazuri.

Kwa muda wa siku nane,Waendeshabaiskeli walioshiriki  mbio za Tour du Rwanda  ya mwaka huu  ilikuwa ni  umbali  wa kilomita 740 kote nchini.

Timu za Afrika hazikufua dafu mwaka  huu licha ya kwamba Eritrea imetawazwa kuwa timu bora katika shindano hili lakini hakuna mwafrika aliyethubutu kushindi hatua hata moja.

Aidha, Rwanda itakuwa ni mwenyeji wa mashindano ya dunia ya mbio za baiskeli  ‘’ UCI World Championships 2025’’. Itakuwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika nchini Rwanda na barani Afrika kwa jumla.

Mshindi wa Tour du Rwanda 2024 Joseph Blackmore

Christopher Karenzi


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *