Maandalizi ya Mashindano ya Dunia ya Sitting Volleyball 2026

Share Now

Na Christopher Karenzi

Jumla ya timu 32 zitashiriki mashindano hayo, ambapo timu 16 za wanawake na timu 16 za wanaume zitacheza katika hatua ya awali kabla ya kuingia hatua za mtoano.

Kwa mujibu wa Rais wa Chama cha Michezo ya watu wenye ulemavu nchini Rwanda (NPC Rwanda), Bizimana Dominique, ratiba ya mashindano ya 2026 WPV Sitting Volleyball World Championship itakayofanyika katika jiji la Hangzhou, China, kuanzia tarehe 10 hadi 17 Julai 2026, tayari imekamilika na kuonesha timu zitakazoshiriki katika hatua ya awali ya mashindano (Preliminary Round).

Mashindano haya yanaandaliwa na World ParaVolley na yanatarajiwa kukutanisha timu bora za sitting volleyball kutoka mabara mbalimbali duniani, zikishindania ubingwa wa dunia katika makundi ya wanaume na wanawake.

Katika upande wa wanawake, nchi zitakazoshiriki ni: China, Kenya, Canada, Netherlands, Hungary, Thailand, Brazil, Rwanda, Iran, Germany, Ukraine, Slovenia, Japan, Italy, France na United States.

Kwa upande wa wanaume, timu zitakazoshiriki ni: China, Thailand, Egypt, Rwanda, Brazil, Iraq, Bosnia and Herzegovina, Japan, Germany, Canada, United States, Ukraine, Kazakhstan, Croatia, Iran na Poland.

Ushiriki wa Rwanda katika mashindano haya ni hatua muhimu katika kuendeleza mchezo wa sitting volleyball nchini. Timu za taifa za wanaume na wanawake zimekuwa zikionyesha maendeleo katika mashindano ya kimataifa, na ushiriki wao katika mashindano ya dunia unatarajiwa kuongeza uzoefu na ushindani kwa wachezaji.

Mashindano haya yatatoa fursa kwa timu mbalimbali kupima uwezo wao dhidi ya mataifa yenye uzoefu mkubwa katika mchezo huu, huku yakichangia pia kukuza mchezo wa sitting volleyball duniani.

Rais wa NPC Rwanda Bizimana Dominique

Viongozi wa michezo nchini Rwanda wanaamini kuwa ushiriki katika mashindano haya ya dunia utasaidia kuongeza kiwango cha wachezaji, kuimarisha maandalizi ya baadaye na kuendelea kuiwakilisha vyema nchi katika majukwaa ya kimataifa.

Mashindano ya 2026 WPV Sitting Volleyball World Championship yanatarajiwa kuwa miongoni mwa mashindano makubwa ya michezo ya walemavu duniani, yakileta pamoja timu bora na kuonesha maendeleo ya mchezo huo katika ngazi ya kimataifa.

Ratiba  ya mwaka  2026 WPV Sitting Volleyball World Championship itakayofanyika jijini Hangzhou, China (10–17 Julai 2026), hizi ndizo timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia katika hatua ya awali (Preliminary Round).

Kwa jumla ni timu 32 (16 wanawake + 16 wanaume) zitashiriki


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *