CEO Christian Gakwaya : Wawekezaji   waonyesha dhamira  ya kuwekeza zaidi katika sekta ya michezo.

Share Now

Na Christopher Karenzi

Mara baada ya  kutamatisha mkutano wa wa siku mbili wa SportsBiz Africa, jijini Kigali  tarehe 10 Septemba 2025, viongozi mbalimbali  kutoka mataifa tofauti, Mawaziri, wadau wa michezo, wakufunzi,  wameazimia kuwa na sauti moja ya kuimarisha michezo na kuwekeza mali kwenye sekta ya michezo.

Mkurgenzi mtendaji wa mradi SportsBiz Africa Christian Gakwaya baada ya Kongamano alizungumzia kuhusu mashindano ya Gufu yaliyofanyika jijini Kigali.

‘’Nikirejelea sana mchezo wa gofu, ni miongoni mwa malengo ya SportsBiz  kuhakikisha inafanikisha shughuli zinawafikia watu. Katika gofu, kuna mchezaji Mnyarwanda aitwaye Celestin Nsanzuwera, ambaye alishinda mashindano ya gofu.

Mashindano  tuliyoleta hapa ni miongoni mwa yale yanayowapa wachezaji nafasi ya kupata alama zinazotambulika kimataifa. Ushindi wake umemruhusu kupanda moja kwa moja kwenye viwango vya ubora vya dunia’’.  Alisema Gakwaya.

CEO wa SportsBiz Africa Christian Gakwaya

Kuhusu suala la kuwekeza, Bwana Gakwaya  amesema  ‘’Baadhi ya wawekezaji walioshiriki kwenye kongamano hili wameonyesha utayari wa kuwekeza, lakini wanataka sasa kuwe na mfuko wa uwekezaji utakaokusanya fedha zao na kisha uwekezwe kwa pamoja kwa ufanisi zaidi’’. Alisema Gakwaya

Wakati huo huo, baadhi ya wawekezaji walioshiriki kwenye kongamano la michezo lililoambatana na mashindano haya wameonesha dhamira ya kuwekeza zaidi katika sekta ya michezo.

Aidha Hamim Yahaya Rais na mwanzilishi wa kituo cha  shule cha vijana wanaocheza soka Dream Team Football Academy ya jijini Mwanza, Tanzania  amesema kwamba  amenufaika mengi sana katika Kongamano la siku mbili jijini Kigali ‘’Niliweza kusikiliza Rais wa Yanga Africans Eng. Hersi Said, akitoa changamoto sehemu Yanga iliyopitia na mpaka sasa ilivyo kwa kweli nimejifunza mambo mengi sana. Hamim amedokeza haya  ‘’Nimeona kwamba inahitaji uwekezaji katika mpira wa kisasa ili kuhakikisha kwamba hizi timu  zinakuwa zinapata mapato makubwa ambayo yatawezesha kuwa na wachezaji wawe kwenye viwango cya kupata vitita kwa manufaa yao, jamii nzima na kwetu sisi tunaposhiriki michezo’’. Amesema Hamimkurugenzi Mtendaji Mankaito Pius Ballemwa CEO wa kituo hicho amebaini kwamba mchezo wa soka wa sasa unahitaji uwekezaji ‘’ Ili uweze  kutengeneza ushindani wa kibiashara unatakiwa kuwekeza tukubali tupokee wafadhili ili tuweze kupiga hatua kwenye mpira wetu wa Afrika na Tanzania kwa jumla’’.

Hamim Yahaya (Kulia) Rais na mwanzilishi wa kituo cha Dream Team Football Academy na Mankaito Pius Ballemwa CEO Dream Team Football Academy Mwanza, Tanzania

Sekta ya michezo nchini Rwanda imepata msukumo mpya baada ya kuzinduliwa kwa SBA Connect, jukwaa jipya la ajira na maendeleo ya kazi, lililoundwa mahsusi kwa sekta ya michezo.Umurava, kampuni ina uzoefu mkubwa katika sekta ya ajira na teknolojia, imewezesha jukwaa hili kwa kutoa nguvu ya kidijitali. Tayari imeorodhesha zaidi ya kampuni 400, watu 1,300 wamepata ajira kupitia mfumo wake, na nafasi za kazi zaidi ya 5,000 zimetangazwa. Aidha, imejenga hifadhi data ya zaidi ya vipaji 20,000 katika nyanja za kidijitali na biashara

SBA Connect ndilo jukwaa la kwanza la aina yake nchini Rwanda, likitoa nafasi ya kipekee kwa mashirika na wataalamu wa michezo kukutana. Kupitia mfumo huu, watendaji na vijana wenye vipaji wataweza kupata fursa ambazo awali zilikuwa hazijulikani au vigumu kufikiwa.

Kwa kuanzia, SBA Connect inajumuisha makundi 14 tofauti, kuanzia riadha na ukocha, hadi masuala ya teknolojia, masoko, fedha, na uendeshaji. Pia inafungua njia rasmi za kazi katika usimamizi wa matukio, mazoezi ya mwili (fitness), na vyombo vya habari. Kwa hatua hii, sekta ya michezo nchini inachukuliwa kama sehemu muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi, badala ya kubaki kwenye pembe za burudani pekee.

Kwa Rwanda yenye idadi kubwa ya vijana, SBA Connect inatoa matumaini mapya. Vijana wengi wanatafuta njia mbadala za kazi nje ya taaluma za kiasili, na michezo sasa inachukuliwa kama chaguo halali la kitaaluma. Mbali na ajira za moja kwa moja, SBA Connect inatarajiwa kuchangia ukuaji wa sekta nyingine zinazohusiana na michezo kama utalii, vyombo vya habari, na uzalishaji. Pia litainua viwango vya taaluma katika mashindano na mashirika ya michezo nchini.

Kwa mujibu wa SportsBiz Africa, michezo siyo tu burudani bali ni injini ya maendeleo endelevu barani Afrika. Kupitia SBA Connect, Rwanda sasa imejiweka kwenye ramani kama nchi inayotumia michezo si tu kwa ushindani, bali pia kama chanzo cha ajira na maendeleo ya uchumi.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *