{"id":5606,"date":"2025-12-16T19:11:34","date_gmt":"2025-12-16T19:11:34","guid":{"rendered":"https:\/\/brightafrica.rw\/?p=5606"},"modified":"2025-12-16T19:11:35","modified_gmt":"2025-12-16T19:11:35","slug":"mkuu-wa-sekta-ya-fedha-asiimwe-eadb-ni-mshirika-imara-wa-maendeleo-kwa-rwanda","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/2025\/12\/16\/mkuu-wa-sekta-ya-fedha-asiimwe-eadb-ni-mshirika-imara-wa-maendeleo-kwa-rwanda\/","title":{"rendered":"Mkuu wa Sekta ya Fedha Asiimwe : EADB ni mshirika imara wa maendeleo kwa Rwanda"},"content":{"rendered":"\n<p><strong>Na Christopher Karenzi<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p><strong><a href=\"mailto:chriskarenzi@gmail.com\">chriskarenzi@gmail.com<\/a><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Jijini Kigali <strong>Jumanne tarehe 16 Desemba 2025, <\/strong>\u00a0kumefayika mkutano wa siku moja ambao umeandaliwa na <strong>Benki ya Maendeleo ya Afrika ya Mashariki ( EADB).<\/strong> Mkutano huu umeandaliwa chini ya kaulimbiu isemayo:\u00a0<strong><em>\u201c<\/em><\/strong><em>Mchango wa Ufadhili wa EADB katika Mageuzi ya Kijamii na Kiuchumi ya Rwanda.\u201d<\/em>\u00a0Lengo ni kuangazia mchango wa Benki katika maendeleo ya Rwanda kupitia ufadhili jumuishi na wa kimkakati.<\/p>\n\n\n\n<p>East Africa Development Bank (EADB) ina mpango wa kutoa mikopo kwa jumla ya Milioni 150 of US $ kwa miradi mbalimbali mwaka ujao wa 2026<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"683\" src=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/MINECOFIN-1024x683.jpeg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5608\" srcset=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/MINECOFIN-1024x683.jpeg 1024w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/MINECOFIN-300x200.jpeg 300w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/MINECOFIN-768x512.jpeg 768w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/MINECOFIN.jpeg 1080w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p>                                                                                                           Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha nchini Rwanda, Bw. Herbert Asiimwe,<\/p>\n\n\n\n<p>Akizungumza katika kikao cha wadau kilichoandaliwa na Benki hiyo, &nbsp;Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha nchini Rwanda, Bw. Herbert Asiimwe, aliyemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango ya Kiuchumi (MINICOFIN) nchini Rwanda, &nbsp;amesema kuwa EADB imekuwa mshirika imara wa maendeleo kwa Rwanda kwa miaka kadhaa.<\/p>\n\n\n\n<p><em>\u201cProgramu za ufadhili za EADB zimeimarisha sekta muhimu za uzalishaji kama vile viwanda, kilimo, usafirishaji, mali isiyohamishika, biashara, makazi na sekta ya SME, hivyo kuchochea shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi kote Rwanda<\/em>,\u201d Amesema Bw. Asiimwe. Amebaini kuwa, <em>\u201cUwekezaji wa EADB umechangia moja kwa moja katika malengo ya kipaumbele ya Maendeleo Endelevu ya Rwanda kwa kuunga mkono shughuli za kuzalisha kipato na kuleta matokeo yanayolingana kikamilifu na Dira ya Rwanda 2050, inayolenga ukuaji shirikishi, endelevu na unaoongozwa na sekta<\/em>.\u201d<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa historia fupi, Benki hiyo ilianza mwaka 1967 na wanachama wa Jumuiya ya mwanzo\u00a0 ya Afrika ya Mashariki\u00a0 kabla haijavunjika. Benki iliendelea kuwepo pamoja na kwamba \u00a0Jumuiya ilikuwa imevunjika, Kwa mujibu wa Bwana Benard, Jumuiya\u00a0 ilipoanzishwa upya Benko imeendelea kuwepo na Makao makuu yako jijini Kampala, \u00a0Uganda.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"683\" src=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/EADB-Ag.-Director-General-Benard-Mono-1024x683.jpeg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5609\" srcset=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/EADB-Ag.-Director-General-Benard-Mono-1024x683.jpeg 1024w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/EADB-Ag.-Director-General-Benard-Mono-300x200.jpeg 300w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/EADB-Ag.-Director-General-Benard-Mono-768x512.jpeg 768w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/EADB-Ag.-Director-General-Benard-Mono.jpeg 1280w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p>                                                                                          <strong>Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ya Mashariki \u00a0\u00a0EADB , Bw. Benard<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>                                                                      <strong>Jukumu la benki hiyo ni nini hasa?<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p><strong>Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ya Mashariki \u00a0(\u00a0EADB) , Bw. Benard amesema : <em>\u2018\u2019Jukumu lake\u00a0 kuu ni kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Afrika ya Mashariki na <\/em><\/strong><strong><em>EADB ni\u00a0 mojawapo ya taasisi\u00a0 ambazo zinaorodheshwa\u00a0 kama Taasii za Jumuiya\u2019\u2019 .<\/em><\/strong><\/p>\n\n\n\n<p><strong>Mwaka 2008, Rwanda ilijiunga rasmi kama mwanachama, mwanahisa wa Benki ya Maendeleo ya ya Afrika ya Mashariki.<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Kwa wakati huu sasa kuna wanahisa wanne ikiwa ni pamoja na Serikali za Tanzania,Kenya Uganda na Rwanda. Kwa mujibu wa Bwana Benard, kuna mpango wa kwenda nchini Burundi kuongea na nchi jirani ya Burundi ili kwa miaka ijayo waanzishe Benki hiyo ya Maendeleo.  Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) imetoa kwa jumla dola za Marekani milioni 33 (sawa na takribani faranga za Rwanda bilioni 48) kwa taasisi nne washirika nchini Rwanda tangu kuzinduliwa kwa Mpango wake wa SME wa mwaka 2024.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"683\" src=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/Bi-Kaberuka-kushoto-1-1024x683.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5610\" srcset=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/Bi-Kaberuka-kushoto-1-1024x683.jpg 1024w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/Bi-Kaberuka-kushoto-1-300x200.jpg 300w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/Bi-Kaberuka-kushoto-1-768x512.jpg 768w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/Bi-Kaberuka-kushoto-1.jpg 1080w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p>                         Bi Kaberuka (kushoto) ni miongoni mwa akina mama walionufaika kupata mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ya Mashariki <strong>\u00a0(EADB)<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Fedha hizo zimepitishwa kupitia taasisi za kifedha washirika ambazo ni Benki ya Maendeleo ya Rwanda (BRD), Duterimbere IMF Plc, AB Rwanda Plc na Letshego Rwanda. Ufadhili huo umeziwezesha biashara ndogo na za kati (SME) katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, viwanda, biashara, makazi na usafirishaji.Hatua hiyo imefikia hatua ya kubuni \u00a0zaidi ya ajira 7,000, zikiwemo ajira za kudumu zaidi ya 4,000 na ajira za muda zaidi ya 3,000. Asilimia 40 ya ajira hizo zimewanufaisha wanawake.<\/p>\n\n\n\n<p>Malipo hayo ni sehemu ya Mfuko wa SME wa EADB wa thamani ya dola za Marekani milioni 36 (takribani faranga za Rwanda bilioni 47.2), uliozinduliwa Julai 2024, kwa lengo la kutoa mikopo kwa zaidi ya SME 500 kote nchini.<\/p>\n\n\n\n<p><strong>Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EADB, Bw. Benard Mono,<\/strong> amesisitiza kuwa Benki hiyo inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Biashara ndogo, ndogo na zile za kati (MSME) katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi ndani ya nchi wanachama, ndiyo maana imejizatiti kuimarisha upatikanaji wa huduma za kifedha na ujumuishaji wa kifedha kwa MSME. \u201c<em>Kwa kuwa sisi ni Benki ya maendeleo ya kikanda inayomilikiwa kwa pamoja na nchi wanachama, tunajivunia kuwa washirika wa muda mrefu wa kila nchi mwanachama, huku tukielekeza ufadhili wetu kulingana na vipaumbele vya kitaifa.<\/em> <\/p>\n\n\n\n<p><em>Wajibu wetu kama EADB nchini Rwanda na katika ukanda mzima si kutoa mtaji pekee, bali pia kuchochea mabadiliko ya kimfumo, ili kubadilisha fedha kuwa tija, uthabiti na fursa,\u201d alisema Bw. Mono<\/em>.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"683\" src=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/Wajumbe-wa-EADB-1-1024x683.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5611\" srcset=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/Wajumbe-wa-EADB-1-1024x683.jpg 1024w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/Wajumbe-wa-EADB-1-300x200.jpg 300w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/Wajumbe-wa-EADB-1-768x512.jpg 768w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/Wajumbe-wa-EADB-1.jpg 1080w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p>                                                                                    Wajumbe  wa  EADB <\/p>\n\n\n\n<p>Bw. Mono ameongeza kuwa, kwa kuzingatia Dira ya Rwanda 2050, wajibu wa EADB utakuwa kufadhili kile ambacho Rwanda inapaswa kuwa kesho taifa shirikishi, lenye uthabiti na lenye ustawi kwa vizazi vya sasa na vijavyo.<em>\u201cKwa pamoja, hatufadhili miradi pekee, bali tunajenga mustakabali wa Rwanda na kubadilisha maisha, mtu mmoja baada ya mwingine,\u201d <\/em>Ameongeza.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"683\" src=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/EADB-Member-1024x683.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5612\" srcset=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/EADB-Member-1024x683.jpg 1024w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/EADB-Member-300x200.jpg 300w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/EADB-Member-768x512.jpg 768w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/EADB-Member.jpg 1280w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p>                                                                                                           Dr James Tumusiime &#8211; EADB Board Director<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"683\" src=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/MBUNDU-1024x683.jpeg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5613\" srcset=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/MBUNDU-1024x683.jpeg 1024w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/MBUNDU-300x200.jpeg 300w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/MBUNDU-768x512.jpeg 768w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/MBUNDU.jpeg 1080w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p>                                                                                                      Faustin Mbundu &#8211; EADB Board Director<\/p>\n\n\n\n<p>Benki hiyo ya Maendeleo ya Afrika ya Mashariki (EADB) inao mpango wa kujenga  ofisi tawi  katika Mtaa wa Nyarutarama, jijini Kigali Rwanda  mwaka ujao 2026 kwani wakati huu wanakodi ofisi ya kufanyia kazi.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Na Christopher Karenzi chriskarenzi@gmail.com Jijini Kigali Jumanne tarehe 16 Desemba 2025, \u00a0kumefayika mkutano wa siku moja ambao umeandaliwa na Benki<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":5607,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[7],"tags":[],"class_list":["post-5606","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-ubukungu"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/5606","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=5606"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/5606\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":5614,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/5606\/revisions\/5614"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/media\/5607"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=5606"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=5606"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=5606"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}