{"id":5493,"date":"2025-10-31T13:50:26","date_gmt":"2025-10-31T13:50:26","guid":{"rendered":"https:\/\/brightafrica.rw\/?p=5493"},"modified":"2025-10-31T13:53:18","modified_gmt":"2025-10-31T13:53:18","slug":"m23-yapinga-wito-wa-ufaransa-wa-kufunguliwa-kwa-uwanja-wa-ndege-wa-goma","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/2025\/10\/31\/m23-yapinga-wito-wa-ufaransa-wa-kufunguliwa-kwa-uwanja-wa-ndege-wa-goma\/","title":{"rendered":"M23 Yapinga Wito wa Ufaransa wa kufunguliwa kwa uwanja wa ndege wa Goma"},"content":{"rendered":"\n<p><strong>Na Christopher Karenzi<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Muungano wa  &#8221;<strong>Alliance Fleuve Congo (AFC\/M23), <\/strong>kinachodhibiti maeneo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kimepinga tamko la hivi karibuni la Rais wa Ufaransa <strong>Emmanuel Macron, <\/strong>aliyetoa wito wa kufunguliwa tena <strong>uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Goma.<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>M23 imesema uamuzi huo \u201chaumbatani na hali halisi ya mambo yanayoendelea Goma, na umechukuliwa bila kushauriana na pande husika.\u201d<\/p>\n\n\n\n<p>Katika taarifa iliyotolewa na <strong>Corneille Nangaa<\/strong><strong>,<\/strong> Kiongozi wa  muungano wa AFC\u2013M23, kundi hilo lilionyesha mshangao kwamba tangazo hilo lilitolewa mjini <strong>Paris<\/strong><strong>,<\/strong> wakati wa mkutano wa kimataifa uliojadili misaada ya kibinadamu kwa eneo la <strong>maziwa Makuu<\/strong>, bila kufanyika kwa mashauriano au tathmini ya kina ya hali ya usalama huko Kivu.<\/p>\n\n\n\n<p>Nangaa amesema: <em>\u201cUamuzi huu umechukuliwa kwa pupa, hauendani na ukweli wa mambo, na haukuzingatia maoni ya AFC\/M23.\u201d<\/em><\/p>\n\n\n\n<p>Rais Macron alitangaza mpango wa kufunguliwa kwa uwanja wa ndege wa Goma &nbsp;<strong>Alhamisi, Oktoba 30<\/strong>, wakati wa mkutano ulioitwa <em>\u201cInternational Conference for Peace and Prosperity in the Great Lakes Region\u201d<\/em> uliofanyika Paris, ambapo aliketi pamoja na Rais wa DR Kongo <strong>F\u00e9lix Tshisekedi<\/strong>, kiongozi wa Togo, na wajumbe kutoka nchi mbalimbali.<\/p>\n\n\n\n<p>Macron alisema uwanja wa ndege wa Goma utafunguliwa tena \u201ckatika wiki chache zijazo\u201d ili kurahisisha safari za ndege za misaada na kufikisha huduma kwa wakazi wa mashariki mwa Kongo wanaoteseka kutokana na vita.<\/p>\n\n\n\n<p>Alisisitiza kwamba hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za <em>\u201ckurejesha miundombinu iliyoharibiwa na kuimarisha shughuli za kibinadamu.\u201d<\/em>Akasema: <em>\u201cKufunguliwa tena kwa uwanja wa Goma kwa ajili ya misaada ya kibinadamu ni hatua muhimu katika kurejesha matumaini na maisha kwa wananchi wa mashariki mwa Kongo. Ufaransa, pamoja na washirika wake, watahakikisha misaada inafika mahali panapohitajika.\u201d<\/em><\/p>\n\n\n\n<p>Macron pia alifichua kwamba jumuiya ya kimataifa tayari imekusanya <strong>euro bilioni 1.5 (\u20ac1.5 billion)<\/strong> kusaidia miradi ya misaada na ujenzi wa kiuchumi katika eneo la Maziwa Makuu, ikiwemo DRC, Rwanda, Burundi, na Uganda. Alizitaka pande zote \u201ckusitisha mapigano na kuruhusu misaada kufika kwa walioathirika.\u201d<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1000\" height=\"665\" src=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/10\/DRC-2.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5495\" srcset=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/10\/DRC-2.jpg 1000w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/10\/DRC-2-300x200.jpg 300w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/10\/DRC-2-768x511.jpg 768w\" sizes=\"auto, (max-width: 1000px) 100vw, 1000px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p>                                                                                                                                                Rais wa  Togo Faure Gnassingb\u00e9<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa upande wake, Nangaa alisema tamko la Macron&nbsp; halina msingi kwani wakati anazungumzia misaada, \u201cjeshi la serikali ya Kongo na washirika wake wanaendelea kushambulia raia, kuvunja viwanda, madaraja, na hata kulenga ndege za misaada.\u201d<\/p>\n\n\n\n<p>Amesema: <em>\u201cNi unafiki kusema uwanja wa ndege utatumika kwa misaada, ilhali wahudumu wa misaada na raia wanaolengwa na misaada hiyo wanashambuliwa kila siku.\u201d<\/em><\/p>\n\n\n\n<p>AFC\u2013M23 pia ililaani kile ilichokiita <em>\u201ckuvuruga uchumi wa raia wa Goma,\u201d<\/em> ikisema benki zimefungwa na wananchi hawawezi kutoa fedha zao, jambo lililoathiri vibaya maisha ya kiraia.<\/p>\n\n\n\n<p>Kundi hilo lilitaja changamoto kadhaa zinazoathiri mchakato wa kurejesha amani, ikiwemo mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (drones) yanayolenga raia, na mashambulizi dhidi ya ndege za misaada katika maeneo ya <strong>Walikale<\/strong><strong><em> na<\/em> <\/strong><strong>Minembwe<\/strong><strong>.<\/strong> Pia lilishutumu serikali ya Kinshasa kwa <em>\u201ckufunga anga\u201d<\/em> katika maeneo yanayodhibitiwa na M23 ili kurahisisha mashambulizi ya kijeshi.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1000\" height=\"563\" src=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/10\/DRC.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5496\" style=\"width:1054px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/10\/DRC.jpg 1000w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/10\/DRC-300x169.jpg 300w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/10\/DRC-768x432.jpg 768w\" sizes=\"auto, (max-width: 1000px) 100vw, 1000px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p>                                                                                                           Rais wa Ufaransa <strong>Emmanuel Macron<\/strong> akiwa pamoja na Rais wa DRC <strong>F\u00e9lix Tshisekedi<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Nangaa alisisitiza kuwa maeneo yanayodhibitiwa na <strong>AFC\u2013M23<\/strong> yana amani na utulivu, huku akituhumu Kinshasa kwa kuendelea \u201ckuchochea vurugu.\u201d<\/p>\n\n\n\n<p>Alishutumu pia makundi yanayojinufaisha kupitia misaada ya kibinadamu, akisema wanatumia mateso ya wakimbizi kwa maslahi ya kisiasa na kifedha, akitaka Ufaransa \u201ckutojenga sera zake juu ya watu wanaotumia mateso ya wengine kujitajirisha.\u201d<\/p>\n\n\n\n<p>Amesema: <em>\u201cUfaransa haipaswi kuwaunga mkono wanaotumia mateso ya watu kwa faida binafsi, bali ifaidi miradi itakayolinda kwa  amani ya kudumu.\u201d<\/em><\/p>\n\n\n\n<p>Taarifa hiyo ilisisitiza kwamba <strong>AFC\u2013M23<\/strong> imejizatiti kuendeleza njia ya amani kupitia mazungumzo, kwa mujibu wa mipango kama ile ya <strong>mazungumzo ya Doha<\/strong>, na ikatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono juhudi za amani za kweli  si zile zinazochochea vita vipya.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Na Christopher Karenzi Muungano wa &#8221;Alliance Fleuve Congo (AFC\/M23), kinachodhibiti maeneo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini mashariki mwa Jamhuri<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":5494,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[4],"tags":[],"class_list":["post-5493","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-politiki"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/5493","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=5493"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/5493\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":5499,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/5493\/revisions\/5499"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/media\/5494"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=5493"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=5493"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=5493"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}