{"id":5182,"date":"2025-09-09T19:33:44","date_gmt":"2025-09-09T19:33:44","guid":{"rendered":"https:\/\/brightafrica.rw\/?p=5182"},"modified":"2025-09-09T20:05:34","modified_gmt":"2025-09-09T20:05:34","slug":"waziri-mukazayire-michezo-inapaswa-kuwa-nguzo-ya-maendeleo-ya-kiuchumi","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/2025\/09\/09\/waziri-mukazayire-michezo-inapaswa-kuwa-nguzo-ya-maendeleo-ya-kiuchumi\/","title":{"rendered":"Waziri Mukazayire:\u00a0 Michezo inapaswa kuwa nguzo ya maendeleo ya kiuchumi."},"content":{"rendered":"\n<p>Na Christopher Karenzi<\/p>\n\n\n\n<p>Jumanne hii tarehe 9 Septemba 2025, jijini Kigali, umefunguliwa rasmi Kongamano la pili la kimataifa la SportsBiz Africa Forum 2025, unaojikita katika kujadili uwekezaji katika michezo barani Afrika.<\/p>\n\n\n\n<p>Tukio hili muhimu limefanyika katika KCC na limevutia wanamichezo wa sasa na wa zamani, wawekezaji pamoja na viongozi mbalimbali wa sekta ya michezo kutoka mataifa mbalimbali ya bara hili.<\/p>\n\n\n\n<p>Akifungua rasmi kongamano hilo,&nbsp; Waziri wa michezo nchini Rwanda &nbsp;Nelly Mukazayire, amesema&nbsp; nchini Rwanda tunaamini kwa dhati kwamba michezo ni kichocheo cha mabadiliko. Michezo huchochea ukuaji wa vipaji, huleta mshikamano wa kijamii, huunda ajira, huchochea sekta za viwanda na kuibua fursa mpya za uwekezaji.<\/p>\n\n\n\n<p>Ndiyo maana tumeboresha na kuwekeza katika miundombinu ya kisasa ya kiwango cha dunia, ikiwemo <strong>BK Arena<\/strong>na <strong>Uwanja wa Amahoro<\/strong>uliokarabatiwa. Vilevile, tumejenga ushirikiano wa kimkakati na vilabu vikubwa vya soka duniani kama <strong>PSG, <\/strong><strong>Arsenal, Atl\u00e9tico de Madrid<\/strong><strong>,<\/strong> pamoja na <strong>Basketball Africa League<\/strong><strong>,<\/strong> ili kufanikisha dira yetu ya kuwa kitovu cha michezo barani Afrika.<\/p>\n\n\n\n<p>Kupitia uandaaji wa matukio makubwa ya kimataifa kama vile <strong>Mikutano Mikuu <\/strong><strong>na Tuzo za FIA, Mkutano wa FIFA<\/strong>, na <strong>Mashindano ya Dunia ya Mbio za Baiskeli (<\/strong><strong>UCI Road World Championships) <\/strong>tumeimarisha sekta ya huduma, tukapanua utalii, tukakuza ubadilishanaji wa kitamaduni, na zaidi ya yote tumeonyesha uwezo mkubwa wa Afrika kwenye jukwaa la dunia.<\/p>\n\n\n\n<p>Lakini mafanikio haya hayahusu tu miundombinu na matukio. Ni pia kuhusu kulea na kukuza vipaji vya ndani vinavyoweza kustawi na kufanikisha ndoto zao, kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi wanamichezo wa kiwango cha juu. Michezo ni injini ya maendeleo ya kweli kwa bara letu.<\/p>\n\n\n\n<p>Na kwa kuwa takribani <strong>asilimia 70 ya watu wa Afrika ni vijana chini ya miaka <\/strong><strong>30<\/strong><strong>, <\/strong>kuwekeza katika michezo maana yake ni kuwekeza katika hazina yetu ya thamani zaidi &nbsp;<strong>vijana wetu<\/strong><strong>.<\/strong><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1000\" height=\"667\" src=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/christian-Gakwaya.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5184\" srcset=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/christian-Gakwaya.jpg 1000w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/christian-Gakwaya-300x200.jpg 300w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/christian-Gakwaya-768x512.jpg 768w\" sizes=\"auto, (max-width: 1000px) 100vw, 1000px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p>                                                                                              Rais wa Shirikisho la mchezo mbio za Magari  nchini Rwanda                                  Gakwaya Christian<\/p>\n\n\n\n<p>Mwenyekiti wa Rwanda Events akiwa pia  Rais wa Shirikisho la mchezo mbio za Magari  nchini Rwanda  Christian Gakwaya, amethibitisha kuwa mkutano huu umezaa matokeo chanya, ukionyesha wazi mchango wake katika kuendeleza uwekezaji na ubunifu katika sekta ya michezo barani Afrika.<\/p>\n\n\n\n<p><strong>Kigali yajivunia kuandaa Kongamano la&nbsp; pili wa uwekezaji katika michezo Barani Afrika<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Mkutano huu, unaoandaliwa na Rwanda Events, una lengo la kuunganisha wadau tofauti wa michezo na uwekezaji ili kuchambua fursa na changamoto zinazokabili bara la Afrika katika kuendeleza michezo kama sekta ya kiuchumi.<\/p>\n\n\n\n<p>Akihutubia washiriki,Waziri wa Michezo wa Rwanda, Nelly Mukazayire, alisisitiza nafasi muhimu ya michezo kama kichocheo cha maendeleo ya taifa na bara kwa ujumla.<em>\u201cMichezo inapaswa kuwa nguzo ya maendeleo ya kiuchumi. Afrika sasa imeanza kuondoka katika mtazamo wa kuzalisha vipaji pekee, bali tunaunda wanamichezo wanaoweza pia kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa jamii na bara lote,\u201d<\/em> alisema.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"819\" src=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/WhatsApp-Image-2025-09-09-at-1.01.33-PM-1-1024x819.jpeg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5189\" srcset=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/WhatsApp-Image-2025-09-09-at-1.01.33-PM-1-1024x819.jpeg 1024w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/WhatsApp-Image-2025-09-09-at-1.01.33-PM-1-300x240.jpeg 300w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/WhatsApp-Image-2025-09-09-at-1.01.33-PM-1-768x614.jpeg 768w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/WhatsApp-Image-2025-09-09-at-1.01.33-PM-1.jpeg 1080w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p>                                                                                                              Waziri wa michezo wa Rwanda Nelly Mukazayire<\/p>\n\n\n\n<p>Waziri Mukazayire ameeleza kuwa ingawa soko la kimataifa la michezo linaendelea kukua kwa kasi, mchango wa Afrika bado ni mdogo sana. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2024, thamani ya soko hilo ilifikia dola bilioni 480, na inatarajiwa kupanda hadi zaidi ya dola bilioni 630 ifikapo mwaka 2028.<\/p>\n\n\n\n<p>Hata hivyo, ameongeza kuwa kiwango cha uwekezaji katika michezo barani Afrika kiko chini ya asilimia 0.5%, ikilinganishwa na mabara mengine ambayo yako wastani wa 2.5%. Kwa mujibu wa Waziri Mukazayire, hali hii inapaswa kuwa changamoto na mwamko kwa bara lote kuongeza jitihada, hasa ikizingatiwa kuwa vijana wanachukua nafasi kubwa katika idadi ya watu wa Afrika.<\/p>\n\n\n\n<p>Mkutano wa <em>SportsBiz Africa Forum 2025<\/em> utaendelea hadi Jumatano, Septemba 10, ambapo washiriki wanatarajiwa kujadili mbinu za kuvutia wawekezaji, kuboresha miundombinu, na kukuza michezo barani Afrika kama injini ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"682\" src=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/Claire-Akamanzi-1024x682.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-5187\" srcset=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/Claire-Akamanzi-1024x682.jpg 1024w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/Claire-Akamanzi-300x200.jpg 300w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/Claire-Akamanzi-768x512.jpg 768w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/Claire-Akamanzi-1536x1024.jpg 1536w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2025\/09\/Claire-Akamanzi-2048x1365.jpg 2048w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p>                                                                              Claire Akamanzi  CEO wa NBA Africa alikuwa miongoni mwa waliohudhiria Kongamano hilo<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Na Christopher Karenzi Jumanne hii tarehe 9 Septemba 2025, jijini Kigali, umefunguliwa rasmi Kongamano la pili la kimataifa la SportsBiz<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":5183,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[9],"tags":[],"class_list":["post-5182","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-imikino"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/5182","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=5182"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/5182\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":5190,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/5182\/revisions\/5190"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/media\/5183"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=5182"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=5182"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=5182"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}