{"id":2414,"date":"2022-07-23T13:29:19","date_gmt":"2022-07-23T13:29:19","guid":{"rendered":"https:\/\/brightafrica.rw\/?p=2414"},"modified":"2022-07-23T13:29:20","modified_gmt":"2022-07-23T13:29:20","slug":"bara-la-afrika-lina-takriban-elfu-nane-mia-tano-sehemu-ya-maeneo-yaliyohifadhiwa-huku-takriban-watu-milioni-mia-tatu-wakitegemea-hifadhi-hizi-kwa-pato-lao-la-kila-siku","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/2022\/07\/23\/bara-la-afrika-lina-takriban-elfu-nane-mia-tano-sehemu-ya-maeneo-yaliyohifadhiwa-huku-takriban-watu-milioni-mia-tatu-wakitegemea-hifadhi-hizi-kwa-pato-lao-la-kila-siku\/","title":{"rendered":"Bara la Afrika lina takriban elfu nane mia tano sehemu\u00a0 ya maeneo yaliyohifadhiwa huku takriban watu milioni mia tatu wakitegemea hifadhi hizi kwa pato lao la kila siku.\u00a0"},"content":{"rendered":"\n<p><\/p>\n\n\n\n<p>Haya ni baadhi ya yaliyozungumzwa&nbsp; katika kongamano la wiki moja kuanzia tarehe 18 hadi 23 Julai 2022 kuhusu hifadhi ya mazingira jijini&nbsp; Kigali.<\/p>\n\n\n\n<p>Kumezinduliwa ripoti ya ambayo inazungumzia&nbsp; jinsi pesa zilizotengwa&nbsp; kwa minajiri ya&nbsp; kuhifadhi, zinawafikia walengwa ambao ni mashirika yanayofanya uhifadhi barani Afrika<\/p>\n\n\n\n<p>Mkurugenzi wa maliasili nchini kenya Njenga Kahiro\u00a0 akiongea kuhusu hii ripoti amesema \u2018\u2019Kwa jumla fedha ambazo zipo\u00a0 ambazo zimetengwa kwajili ya hifadhi duniani, asilimia 1 tu ndiyo inayofikia mashirika ya kiafrika na kwa upande\u00a0\u00a0 wafadhili wengine\u00a0 katika sekta binafsi\u00a0 asilimia 5 hadi 10 peke yake\u00a0 ndio hufikia \u00a0mashirika ya kiafrika. Afrika ni bara ambalo \u00a0lina \u00a0eneo kubwa la viumbe hai ambapo ni \u00a0theruthi tatu\u00a0 ya dunia nzima\u2019\u2019.<\/p>\n\n\n\n<p>Bwana Kahiro amebaini kuwa utakuta kwamba jamii na mashirika ya kiafrika yanapata mgao&nbsp; mdogo sana.<\/p>\n\n\n\n<p>Bara la Afrika lina takriban elfu nane, mia tano sehemu maeneo yaliyohifadhiwa huku takriban watu milioni mia tatu wakitegemea hifadhi hizi kwa pato lao la kila siku.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" src=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2022\/07\/Kahoro-director-683x1024.jpeg\" alt=\"\" class=\"wp-image-2416\" width=\"1036\" height=\"1553\" srcset=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2022\/07\/Kahoro-director-683x1024.jpeg 683w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2022\/07\/Kahoro-director-200x300.jpeg 200w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2022\/07\/Kahoro-director.jpeg 720w\" sizes=\"auto, (max-width: 1036px) 100vw, 1036px\" \/><figcaption>Mkurugenzi Mali asili Njenga Kahiro<\/figcaption><\/figure>\n\n\n\n<p>Hayo yakiarifiwa Rais wa Rwanda Paul Kagame, ijumaa tarehe 22 Julai 2022 alipokea ofisini mwake viongozi mbali mbali walioshiriki mkutano wa kimataifa kuhusu hifadhi za mazingira \u00a0[Africa Protected Areas Congress, APAC].<\/p>\n\n\n\n<p>Mpaka sasa nchini Rwanda kuna hifadhi za mazingira zikiwa kwenye asilimia 37,70 ya nchi pia kuna mpango wa kupanua hifadhi ili kuzidi kujenga uchumi usiobugudhi mazingira.<\/p>\n\n\n\n<p>Ili kudumisha maeneo haya yanahitaji hela ambapo bara la Afrika kwa miaka mingi limetegemea wafadhili.<\/p>\n\n\n\n<p>Kulingana na Muungano wa kimataifa unaosimamia mali asili (IUCN) bara la Afrika lina ukosefu wa dola bilioni mia saba ambayo inahitajika kudumisha hifadhi zilizoko pamoja na viumbe hai.<\/p>\n\n\n\n<p>Hazina ya A-PACT ambayo inaonekana kuwa suluhu inahitaji angalau dola bilioni mia mbili kutekeleza suala hili.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa wiki nzima washiriki wa kongamano hili walikuwa wakijadili uwakilishwaji na kuhakikisha uwepo wa wanajamii kwenye hifadhi wa mazingira haswa&nbsp; ukizingatia kwamba rasilimali za siri ziko kwenye jamii.<\/p>\n\n\n\n<p><strong>Wafanyeje ili uhifadhi uwe endelevu?<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p>Alphonse Mallya ni mkurugenzi wa mipango kaskazini mwa&nbsp; Tanzania amesema kwamba Kuna upatikanaji wa fedha lakini pia na ujuzi wa kitaalamu kwa muda mrefu ambao utasaidia wanajamii wenyewe kuweza kuendeleza&nbsp; shughuli za hifadhi kwenye mazingira yenyewe.<\/p>\n\n\n\n<p>Baadhi ya viongozi wa bara la Afrika wamezindua mpango wa kupunguza kuwategemea wafadhili kuhusiana na suala la uhifadhi wa mazingira na kukabili mabadiliko ya hali ya anga.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika kongamano linalotamatika jumamosi tarehe 23 Julai 2022 mjini Kigali Rwanda, hazina ya Pan African conservation trust &#8211; APACT imezinduliwa na inatarajiwa kulikomboa bara la Afrika katika sekta ya uhifadhi wa mazingira haswa kuhusiana na suala la ukosefu wa fedha&nbsp; za kutosha.<\/p>\n\n\n\n<p>Utaratibu ambao huenda ukafuatwa katika uongozi wa hazina ya A-PACT, ni kamati iliyobuniwa ikifuatiwa na marais wa mataifa ya Afrika.<\/p>\n\n\n\n<p>Kila taifa litachangia katika mfuko huu na mgawanyiko wa fedha hizi kutekelezwa kulingana na tatizo katika taifa Ila fedha hizi hazitafika kwenye mikono ya watu serikalini hata hivyo, uongozi wa matumizi yake utapangwa na wasimamizi wa mataifa, mashirika ya binafsi na mashirika yasiyo ya serikali.<\/p>\n\n\n\n<p><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" src=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2022\/07\/kagame-2-1.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-2417\" width=\"1036\" height=\"689\" srcset=\"https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2022\/07\/kagame-2-1.jpg 1000w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2022\/07\/kagame-2-1-300x200.jpg 300w, https:\/\/brightafrica.rw\/wp-content\/uploads\/2022\/07\/kagame-2-1-768x511.jpg 768w\" sizes=\"auto, (max-width: 1036px) 100vw, 1036px\" \/><figcaption>Rais Kagame akiwa pamoja na viongozi mbali mbali kwenye Ikulu Village Urugwiro<\/figcaption><\/figure>\n\n\n\n<p><strong>Christopher Karenzi<\/strong><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Haya ni baadhi ya yaliyozungumzwa&nbsp; katika kongamano la wiki moja kuanzia tarehe 18 hadi 23 Julai 2022 kuhusu hifadhi ya<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":2415,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[11],"tags":[],"class_list":["post-2414","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-ibidukikije"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2414","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=2414"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2414\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":2418,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2414\/revisions\/2418"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/media\/2415"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=2414"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=2414"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/brightafrica.rw\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=2414"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}